Swali: Baba yangu mgonjwa amekufa kabla ya kukamilisha Ramadhaan. Je, tumfungie yale masiku ambayo hakuyamaliza?
Jibu: Hakuna kinachomlazimu kwa sababu amekufa kabla ya kufunga mwezi mzima. Hakuna ambaye atatakiwa kumfungia. Ikiwa hakufunga masiku yaliyotangulia kutokana na maradhi sugu yasiyotarajiwa kupona, basi atatakiwa kulisha masikini kwa kila siku moja ambayo hakufunga. Na ikiwa maradhi yake sio sugu na akafa kabla ya kukamilisha mwezi, basi hatolipa wala hatolisha chakula.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 32-33
- Imechapishwa: 24/03/2022
Swali: Baba yangu mgonjwa amekufa kabla ya kukamilisha Ramadhaan. Je, tumfungie yale masiku ambayo hakuyamaliza?
Jibu: Hakuna kinachomlazimu kwa sababu amekufa kabla ya kufunga mwezi mzima. Hakuna ambaye atatakiwa kumfungia. Ikiwa hakufunga masiku yaliyotangulia kutokana na maradhi sugu yasiyotarajiwa kupona, basi atatakiwa kulisha masikini kwa kila siku moja ambayo hakufunga. Na ikiwa maradhi yake sio sugu na akafa kabla ya kukamilisha mwezi, basi hatolipa wala hatolisha chakula.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 32-33
Imechapishwa: 24/03/2022
https://firqatunnajia.com/33-baba-mgonjwa-amefariki-kabla-ya-kumalizika-kwa-ramadhaan/