32. Ni lazima kwa mwanafunzi kuyajua mambo haya

Ni wajibu kuamka, kuzinduka na kuielewa dini. Muislamu anaritadi anapofanya moja katika vitenguzi vya Uislamu. Haijalishi kitu hata kama atafanya mambo mengine. Akiwa anamwabudu al-Badawiy, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Zaynab, al-Husan, al-Husayn, ´Aliy na anawaomba msaada, anakufuru. Kusema kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hakutomfaa kitu. Kadhalika atapowaomba Malaika, akawaomba msaada wao au majini anakufuru hata kama anatamka shahaadah. Vivyo hivyo atapoiomba miti, mawe au sanamu. Hivo ndivo walivokuwa wakifanya Quraysh kwa al-´Uzzaa, al-Laat na Manaat.

Ni wajibu kwa muislamu ajifunze na awe juu ya ubainifu katika dini yake. Mshirikina ni mshirikina hata kama atasema hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Kafiri ni kafiri hata kama atasema hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Mpaka pale atapoamini maana yake na kutekeleza haki yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nimeamrishwa kuwapiga vita watu mpaka watakaposema “Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Watapoyasema basi vimesalimika kwangu damu na mali yao isipokuwa kwa haki yake.”

Kadhalika akiwaomba na kuwataka msaada Malaika au majini anakufuru japokuwa atatamka shahaadah. Katika Hadiyth ya Ibn ´Umar imekuja:

“… isipokuwa kwa haki ya Uislamu. Hesabu yao iko kwa Allaah.”

Ni lazima kuhakikisha haki ya Uislamu na haki ya shahaadah ambayo ni kule kulazimiana na dini ya Allaah, atahadhari kutokamana na yale yanayosababisha au yanayosababisha kumkadhibisha Allaah na Mtume Wake. Kwa mfano kuna muislamu anayefanya ´ibaadah aina zote na anaamini yale yote aliyowajibisha Allaah. Lakini anaona kuwa hakuna jambo la kufufuliwa na kukusanywa, hakuna Pepo na Moto, anakufuru kwa mujibu wa wote. Haijalishi kitu hata kama anaswali na anafunga na ni miongoni mwa watu wenye kuabudu zaidi. Kadhalika ikiwa anaamini kila kitu lakini anaona kuwa uzinzi na pombe ni halali, swalah, kufunga Ramadhaan au kwamba kuhiji kwa yule mwenye kuweza sio wajibu anakufuru kwa mtazamo wa wote.

 Lililo la wajibu ni kuzinduka juu ya jambo hili na mwanafunzi awe na ujuzi. Asidanganyike na maneno ya waritadi hawa. Hawa ni wajinga na wapotevu ambao wanayaabudu makaburi, wanawaomba msaada wafu na wakati huohuo wanasema kuwa ni waislamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 111-112
  • Imechapishwa: 26/10/2021