Maamuma kunyamaza baada ya al-Faatihah katika swalah za kusoma kwa sauti

Swali: Baada ya imamu kumaliza kusoma Suurah “al-Faatihah” katika swalah za kusoma kwa sauti ya juu maamuma naye anasoma al-Faatihah. Lakini mimi nawasikia baadhi ya watu wanasoma Suurah fupi baada yake. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Haijuzu kwa mswaliji katika swalah za kusoma kwa sauti ya juu akasoma mbali na al-Faatihah. Bali kilicho cha lazima kwake baada ya hapo ni yeye anyamazie kisomo cha imamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pengine mnasoma nyuma ya imamu wenu?” Tukasema: “Ndio.” Akasema: “Msifanye isipokuwa tu kwa ufunguzi wa Kitabu. Kwani hana swalah kwa ambaye hakuisoma.”

Allaah (Subhaanah) amesema:

وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

“Inaposomwa Qur-aan basi isikilizeni na nyamazeni kimya ili mpate kurehemewa.”[1]

Vilevile amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Akisoma imamu basi nyamazeni.”

Kinachobaguliwa katika hayo ni kisomo cha al-Faatihah peke yake kutokana na Hadiyth iliotangulia na kutokana na kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kwani hana swalah kwa ambaye hakuisoma.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] 07:204

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/233)
  • Imechapishwa: 26/10/2021