32. Hakuwahi kulipa siku anazodaiwa mpaka ameingiliwa na Ramadhaan nyingine

Swali: Nina deni la siku saba za Ramadhaan na hivi sasa kumeshapita mwaka. Ni kipi kinachonilazimu?

Jibu: Ikiwa umechelewesha pasi na udhuru, basi utatakiwa kulipa na kulisha chakula kwa kila siku iliyokupita. Na ikiwa ni kutokana na udhuru, basi hakuna kinachokulazimu isipokuwa tu kulipa masiku yako.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 32
  • Imechapishwa: 24/03/2022