Swali: Kuna mwanamke aliacha kufunga miaka mingi wakati alipokuwa mdogo. Isitoshe hajui ni lini ilimjia ada yake ya mwezi. Ni kipi kinachomlazimu hivi sasa?

Jibu: Mwanamke analazimika kufunga wakati anapobaleghe kwa hedhi, kuota au aakafikisha miaka kumi na tano. Katika hali hii anapaswa kuanzia ule umri wa chini kabisa na afunge yale masiku ambayo hakufunga. Aidha anatakiwa kulisha chakula masikini 1.5 kg ya mchele au ngano kwa kila siku iliyompita.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 31
  • Imechapishwa: 24/03/2022