Swali: Kuna mwanamke alijiwa na hedhi akiwa na miaka 13. Ikampitikia miaka minne ya Ramadhaan bila kufunga kwa sababu ya ujinga wake. Alikuwa akiishi mashambani. Alikuwa haswali katika kipindi hicho. Hivi sasa ana miaka 38 na ana tatizo la maambukizi katika ya mfumo wa mkojo. Nini anachotakiwa kufanya? Je, analazimika kufunga au kulisha chakula? Aidha amepanga kuhiji mwaka huu.

Jibu: Analazimika kufunga hiyo miaka mine iliyompita na kulisha masikini kwa kila siku moja iliyompita, kwa sababu imempita pasi na udhuru. Vilevile anatakiwa kutubu kwa Allaah. Hata hivyo jambo hilo halimzuii kuhiji.

Kuhusu kuacha swalah katika kipindi ulichotaja, basi inakutosha kutubu kwa Allaah tawbah ya kweli. Hahitajii kuzilipa kutokana na ugumu wa jambo hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 31
  • Imechapishwa: 24/03/2022