29. Kuacha kufunga kwa sababu ya unyonyeshaji na ujauzito

Swali: Ni lazima kwa mjamzito na mnyonyeshaji kulipa masiku yaliyowapita Ramadhaan wakila kwa sababu ya kuchelea juu ya mtoto? Nimewasikia baadhi ya ndugu wakisema kuwa haiwalazimu kwao kufanya hivo kwa sababu wanaingia ndani ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ

“Na kwa wale wanaoiweza lakini kwa tabu basi watoe fidia: kulisha masikini.”[1]

Jibu: Ni lazima kwao kulipa masiku yao pamoja na kumlisha masikini kwa kila siku moja iliyowapita kwa sababu ya kule kuacha kwao kufunga kwa ajili ya mtoto. Kuhusu msafiri na mwenye hedhi wanalazimika kulipa masiku hayo pasi na kulisha.

[1] 2:184

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 31
  • Imechapishwa: 24/03/2022