32 – Yahyaa bin ´Abdil-Hamiyd ametuhadithia: Sulaymaan bin Bilaal ametuhadithia, kutoka kwa ´Umaarah bin Ghaziyyah, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Aliy bin al-Husayn, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

البخيل ن ذكرت عنده فلم يصلِّ عليَّ

”Bakhili ni ambaye nitatajwa mbele yake asiniswalie.”[1]

Allaah amsifu na amsalimishe kikwelikweli.

[1] Swahiyh kupitia ya kabla yake. Ameipokea Ahmad (1/201), at-Tirmidhiy, imesahihishwa na Hibbaan, al-Haakim (1/549) na at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” kupitia kwa Sulaymaan bin Bilaal. al-Haakim amesema kuwa cheni ya wapokezi ni Swahiyh na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Wanamme wake ni wanamme wa Muslim mbali na ´Abdullaah bin ´Aliy bin al-Husayn. Kuna wengi ambao wameipokea kutoka kwake na Ibn Hibbaan akamzingatia kuwa ni mwaminifu. Hata hivyo kuna tofauti juu ya cheni yake aliyosimulia kutoka kwa ´Umaarah bin Ghaziyyah. Baadhi wameisimulia kwa cheni ya wapokezi isiyokuwa na Swahabah na wengine wameisimulia kwa cheni ya wapokezi yenye kuungana. Sahihi ni hili la mwisho – Allaah akitaka. Aidha kuna Hadiyth inayoitia nguvu iliyopokelewa na Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). al-Fayruuzaabaadiy amemnasibibishia nayo an-Nasaa’iy akasema:

”Hadiyth hii ni Swahiyh.” (ar-Radd ´alaal-Mu´taridhwiyn (1/39 – muswada)).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 10/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy