31. Hadiyth ”Bakhili ni yule ambaye… “

31 –  Ismaa´iyl bin Abiy Uways ametuhadithia: Kaka yangu amenihadithia, kutoka kwa Sulaymaan bin Bilaal, kutoka kwa ´Amr bin Abiy ´Amr, kutoka kwa ´Aliy bin Husayn, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن البخيل لمن ذكرت عنده فلم يصلِّ عليَّ

”Bakhili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake asiniswalie.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni nzuri. Wanamme wake ni wanamme wa al-Bukhaariy. Kuna machache juu ya al-Ismaa´iyl, lakini haidhuru. Ndugu yake jina lake ´Abdul-Hamiyd bin ´Abdillaah Abu Bakr. Ameipokea an-Nasaa’iy na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake. Imepokelewa kwa njia nyingine kutoka kwa ´Aliy bin Husayn itakayokuja baada yake. Hakuna tofauti kati ya njia hizo mbili. Sulaymaan bin Bilaal yuko katika cheni zote mbili, moja wapo ni kutoka kwa ´Amr bin Abiy ´Amr na nyingine ni kutoka kwa ´Umaarah bin Ghaziyyah, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Aliy, kutoka kwa al-Husayn.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 41
  • Imechapishwa: 10/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy