30. Hadiyth ”Swalini majumbani mwenu… ”

30 – Ibraahiym bin Hamzah ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Muhammad ametuhadithia, kutoka kwa Suhayl, ambaye amesimulia:

”Nilikuja kumsalimia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hasan bin Husayn[1] alikuwa anakula chakula cha jioni kwenye nyumba ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akaniita na nikamwendea. Nikasema: ”Sogea karibu ule chakula cha jioni.” Nikasema: ”Sitaki.” Akasema: ”Ni kwa nini nakuona umesimama?” Nikasema: ”Nimesimama kwa ajili ya kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Akasema: ”Unapoingia msikitini, basi mtolee salamu.” Kisha akasema: ”Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

صلوا في بيوتكم ولا تجعلوا بيوتكم مقابر، لعن الله يهود، اتخذوا قبور أنبيائهم مساجد ، وصلوا عليَّ فإن صلاتكم تبلغني حيثما كنتم

”Swalini majumbani mwenu na wala msiyafanye makaburi yenu kuwa makaburi. Allaah awalaani mayahudi, wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni misikiti. Niswalieni. Kwani hakika du´aa zenu hunifikia popote mnapokuwa.”[2]

[1] Namna hii ndivo imekuja katika ile ya asili. Katika maelezo ya chini imekuja ”Sahihi ni Hasan bin Hasan”.

[2] Swahiyh. Tazama Hadiyth (20).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 10/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy