Swali 31: Wajumbe wa Wanusuraji walikuwa wangapi?

Jibu: Ujumbe wa kwanza ulikuwa na watu sita kutoka katika kabila la Khazraj. Wakakubali ujumbe wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kisha wakawalingania watu wa kabila lao katika ujumbe huohuo ambapo ujumbe wa pili ulikuwa na watu wawili kutoka katika kabila la Aws na kumi kutoka katika Khazraj. Hicho ndicho kilikuwa kiapo cha kwanza cha ´Aqabah. Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawatumia Musw´ab ili kuwafunza dini. Matokeo yake jamaa zao wote wakaingia katika Uislamu.

Mwaka uliofuatia wakawa wajumbe 73 wanamme na wanawake wawili. Hichi kilikuwa kiapo cha pili cha ´Aqabah, kikitambulika pia kama kiapo kikubwa. Kiapo cha wanawake kimetajwa katika Suurah ”al-Mumtahinah”. Kiapo hicho kilikuwa pamoja na kumlinda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na yale wanayowalinda wana na familia zao na kwamba malipo yao ni Pepo.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 27/09/2023