Swali: Je, mtu anapata dhambi za wanaomfuata hata baada ya kutubu ikiwa alikuwa mpotofu kisha akaongoka?

Jibu: Kunatarajiwa kwake kusalimika – Allaah akitaka. Akitubu, basi – Allaah akitaka – kunatarajiwa kwake kusalimika. Kwa sababu tawbah inafuta madhambi ya kabla yake. Hata hivyo ni lazima kwake kubainisha kujirejea kwake.

Swali: Wako waliosema kuwa anapata dhambi za wanaomfuata hata baada ya kutubu kutokana na Hadiyth ya mwana wa Aadam ambaye alitubu na juu yake anabeba mzigo wa madhambi wa wanaomfuata.

Jibu: Hainidhihirikii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kutubu juu ya dhambi ni kama hana dhambi yoyote.”

Tawbah inafuta yaliyo kabla yake. Mtoto wa Aadam hatujui kama alitubu au hakutubu? Je, wewe una khabari yoyote kwamba alitubia?

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22975/هل-يلحق-المفسد-بعد-توبته-وزر-من-تبعه
  • Imechapishwa: 27/09/2023