Swali: Kuna mtu leo amekula kiapo, kesho akala kiapo, kesho yake akala kiapo. Je, kafara moja inatosha?

Jibu: Ikiwa ni juu ya kitu kimoja.

Swali: Viapo vya kutofautiana?

Jibu: Unafahamu au hufahamu? Kwa mfano mtu anaapa hii leo kwamba hatomzungumzisha fulani, kesho akaapa kwamba hatomzungumzisha mtu mwingine ambaye anaitwa Zayd, akaapa kwamba hatomzungumzisha ´Uqbah na akaapa kwamba hatomzungumzisha Sa´iyd. Hivi ni viapo vitatu. Kila kimoja katika viapo hivi kina kafara yake. Umefahamu? Miongoni mwa sura zake zingine: akaapa tena kwamba hatomzungumzisha fulani. Hiki ni kiapo cha kwanza. Kiapo cha pili akaapa kwamba hatomtembelea fulani. Matembezi ni tofauti na uzungumzishaji. Kiapo cha tatu akasema kwamba hatokula chakula chake. Hivi ni viapo vitatu ambapo kila kimoja katika hivo kuna kafara yake. Umefahamu au bado?

Mwanafunzi: Ndio. Allaah akujaze kheri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22972/هل-تتعدد-الكفارة-بتعدد-الايمان-واختلافها
  • Imechapishwa: 27/09/2023