Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ngazi ya kwanza: Uislamu una nguzo tano: Kushuhudia ya kwamba hapana mungu anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji Nyumba ya Allaah tukufu.

MAELEZO

Uislamu una nguzo tano: Kushuhudia ya kwamba hapana mungu anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji Nyumba ya Allaah tukufu. Imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uislamu umejengwa katika matano: Kushuhudia ya kwamba hapana mungu anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji nyumba.”[1]

[1] al-Bukhaariy (08) na Muslim (16).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 40
  • Imechapishwa: 08/01/2017