Swali: Ni yapi makusudio ya hawa kutofautisha Shari´ah kati ya mambo ya dhahiri na uhakika wa ndani?

Jibu: Wanachokusudia ni kutoshikamana na yale mambo ya dhahiri. Wao wanafuata yale mambo ya ndani. Mnawajua Baatwiniyyah ambao wanasema Shari´ah ina mambo ya dhahiri na ya ndani. Wasiokuwa wasomi wanatakiwa kufuata yale mambo ya dhahiri. Kuhusu wao wanadai kuwa wanafuata yale mambo ya ndani. Wanapotosha maana ya swalah, zakaah na maamrisho mengine ya dini na huku wanadai kuwa ndio maana yake ya ndani. Wanadai kuwa hakuna anayejua mtindo huo isipokuwa wao tu. Ndio maana wakaitwa “Baatwiniyyah”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2053
  • Imechapishwa: 08/01/2017