Baada ya Allaah (Ta´ala) kubainisha yale ambayo mwanamke anapaswa kuyafunika katika mapambo yake mbele ya wanamme wa kando naye na wale ambao anafaa kuwaonyesha nayo, akamwamrisha katika Aayah nyingine anapotoka nyumbani kwake ayafunike mavazi yake na shungi yake jilbaab. Kwa sababu jilbaab ni yenye kumsitiri na tukufu zaidi kwa maadili yake. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako – na wanawake wa waumini – wajiteremshie Jilbaab zao; hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

Wakati ilipoteremshwa Aayah hiyo wanawake wa ki-Answaar walitoka wakiwa wamejifunika kana kwamba kunguru wameketi juu ya vichwa vyao[2].

[1] 33:59

[2] Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Katika ”ad-Durr” imeegemezwa katika upokezi wa ´Abdur-Razzaaq, ´Abd bin Humayd, Abu Daawuud, Ibn-ul-Mundhir, Ibn Abiy Haatim na Ibn Marduuyah kupitia kwa Umm Salamah ambaye amesema:

”Kutokana na mavazi meusi waliyokuwa wameyavaa.”

Wamefananishwa na kunguru kutokana na mavazi yao meusi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 82-83
  • Imechapishwa: 17/09/2023