Namna hii ndivo wanawake wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baada yake walikuwa wakivaa. Jambo linapelekea katika baadhi ya mambo mengine ya Shari´ah. Maalik na wengineo wamepokea kwamba kijakazi wa Ibraahiym bin ´Abdir-Rahmaan bin ´Awf alimuuliza mke wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

”Mimi ni mwanamke mwenye mkia mrefu na natembea sehemu chafu.” Ndipo Umm Salamah akasema: ”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Inasafishwa na kilicho baada yake.”

Mwanamke mmoja kutoka kabila la Abdul-Ashhal amesema:

”Ee Mtume wa Allaah! Njia yetu ya kwenda msikitini ni chafu. Tufanye nini kunaponyesha?” Akasema: ”Je, baada yake si kuna njia safi zaidi?” Nikasema: ”Ndio.” Akasema: ”Hii ni kwa ajili ya hii.”[1]

Kwa ajili hiyo moja miongoni mwa sharti za waislamu wa mwanzo kwa wake wa wale wanamme wanaolipa kodi waonyeshe miguu yao ili wasijifananishe na wanawake wa Kiislamu, kama ilivyotajwa katika ”Iqtidhwaa´us-Swiraat al-Mustaqim”[2].

[1] Hadiyth hizi mbili amezipokea Abu Daawuud katika ”as-Sunan” yake. Cheni ya wapokezi ya Hadiyth hii ni Swahiyh na imesahihishwa na al-Mundhiriy. Ile Hadiyth ya kwanza ni Swahiyh kupitia zingine na imesahihishwa na Ibn-ul-´Arabiy ilihali Ibn Hajar al-Haytamiy anaona kuwa ni nzuri. Nimeyabainisha hayo katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (407-408).

[2] Kitabu kimeandikwa na Shaykh-ul-Islaam Abul-´Abbas Ahmad bin Taymiyyah al-Harraaniy (Rahimahu Allaah) na ni kitabu kisichokuwa na mfano katika maudhui haya. Nitanukuu kutoka humo faida nyingi katika mlango wa saba. Zingatia mambo yalivyobadilika. Hivi sasa hali imefikia kwamba wanawake wa Kiislamu wanajifakharisha kwa kujifananisha na wale ambao tumekatazwa kujifananisha nao. Haya yote yanafahamisha ukweli wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika mtafuata nyayo za wale waliokuwa kabla yenu hatua kwa hatua, shubiri kwa shubiri, mpaka wakiingia shimo la mburukenge nanyi mtaingia. Wakasema: “E Mtume wa Allaah! Unamaanisha mayahudi na manaswara?” Akasema: “Kina nani wengine?” (al-Bukhaariy (4356) na Muslim (2669))

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 81-82
  • Imechapishwa: 17/09/2023