29. Miguu na nyayo za mwanamke zinapaswa kufunikwa

Katika maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ

”Na wala wasipige miguu yao [wanapotembea] yajulikane yale wanayoyaficha katika mapambo yao.”

kuna dalili juu ya kwamba ni lazima kwa wanawake kuifunika miguu yao, vinginevyo wangeliweza kuonyesha yale mapambo wanayoyaficha, nazo ni zile cheni za miguuni, na hivyo wasingelihitaji kutembea kwa kupiga miguu chini. Lakini ni jambo lisilowezekana kwa sababu linapingana na Shari´ah. Maasi kama haya hayakuwa yenye kutambulika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo walikuwa wakifanya vitimbi vya kutembea kwa kupiga miguu chini ili kuwatambulisha wanamme yale mambo aliyoyaficha na ndio maana Allaah (Ta´ala) akawakataza mambo hayo. Ibn Hazm amesema kwa kujengea yale tuliyoyaweka wazi:

”Yanafahamisha kuwa miguu na muundi vinatakiwa kufunikwa na haifai kuviacha wazi.”[1]

Sunnah inatilia nguvu jambo hilo kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi basi Allaah hatomwangalia siku ya Qiyaamah.” Umm Salamah akasema: ”Wanawake wafanye nini na mikia yao?” Akasema: ”Waiache ishuke shubiri moja[2].” Akasema: ”Hivyo basi itaonekana miguu yao.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Waiche ishuke dhiraa moja na wasizidishe hapo.”[3]

Hadiyth inafahamisha kuwa wanaruhusiwa kuburuza nguo zao kwa sababu ndio kunawasitiri vyema zaidi. al-Bayhaqiy amesema:

”Inafahamisha kuwa analazimika kuifunika miguu yake.”[4]

[1] al-Muhallaa (3/216).

[2] Bi maana kuanzia kwenye nusu ya muundi wake. Maoni mengine yanasema kuanzia kwenye vifundo vya miguu.

[3] at-Tirmidhiy (1731), aliyesema kuwa ni nzuri, na an-Nasaa’iy (5338).

[4] ash-Shawkaaniy ametaja mfano wake katika ”Nayl-ul-Awtwaar”. Wale wenye kuonelea kinyume na wakasema kuwa miguu ya mwanamke sio uchi, kama alivosema al-Mawduudiy, hawana dalili. Jambo la kushangaza ni kuwa amejigonga yeye mwenyewe pale aliposema alipokuwa anatambulisha uchi wa mwanamke akasema:

”Wanawake wameamrishwa kufunika mwili mzima isipokuwa uso na mikono.” (al-Hijaab, uk. 331)

Hakuvua miguu, jambo ambalo ndio sahihi. Ni kipi kilichomfanya kupinda kutokana na hilo?

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 17/09/2023