30. Tofauti kati ya Bid´ah na manufaa yaliyoachiwa

2 – Tafsiri ya pili ni kwamba kila mfumo na njia inayofikisha katika lengo, ambayo ni kuwatengeneza watu, ni sahihi kwa mlinganizi kuitumia kwa sharti dini isiwe imeikataza. Haya ndio yale yanayoitwa manufaa ambayo dini imeyanyamazia na hayakutajwa kwa njia ya kuyazingatia wala kuyakanusha. Haya tunatangamana nayo kwa njia mbili:

1 – Yakawa hayana dalili inayoafikiana na manufaa hayo. Kwa msemo mwingine ni kuwa sababu ikakosa msingi unaozingatiwa katika Shari´ah. Hapo sababu haitosihi. Si sahihi vilevile kujenga hukumu juu yake kwa maafikiano.

2 – Sababu ikawa na msingi wa jumla unaozingatiwa katika Shari´ah hata kama ni pasi na dalili maalum. Haya ndio yale yanayoitwa manufaa yaliyoachiwa (المصالح المرسلة). Katika halii tunatakiwa kuchunguza kama kulikuweko na sababu ya manufaa haya katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au hakukuweko na manufaa. Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kila kitendo ambacho kulikuweko na sababu yake wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lakini hakukifanya, basi itambulike kuwa sio manufaa. Lakini yale ambayo ilipatikana sababu yake baada ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na kumuasi Muumba, basi hayo ni manufaa.”[1]

Hiki kigezo alichothibitisha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) hapa ndio kinachopambanua kati ya Bid´ah na manufaa yaliyoachiwa.

[1] Iqtidhwaa’-us-Swiraatw al-Mustaqiym (2/595).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 15/05/2023