159 – Ziyaad amenihadithia: Ahmad bin Abiyl-Hawaariy amenihadithia: Nimemsikia Abu Sulaymaan ad-Daaraniy akisema:

”Inapendeza zaidi kwangu kuliacha tonge la jioni kuliko kulila na nikasimama usiku mzima.”

160 – Muhammad bin Idriys al-Handhwaliy amenihadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Haani’ amenihadithia: Mis´ar amesema:

Nimekuta jinsi mkate wa bapa unafuku njaa

pamoja na konzi ya maji ya Frati

Chakula kichache kinamsaidia mswaliji,

ilihali chakula kingi kinasaidia matusi

161 – Muhammad bin Idriys amenihadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Haani’ amenihadithia: Sufyaan ath-Thawriy amesema:

Inakutosha kutokana na kile milango ilikuwa imefungwa kwa ajili yake

na wanaohusudu chumvi na vipande vya mikate migumu

Unakunywa na kujilisha kutoka katika maji ya Frati

na unapingana na wale wanaokula ugali kwa siagi

Toa bweu ikiwa wao hawakutoa bweu,

kama vile unaongezeka uzito kutokana na aina mbalimbali za Khabiysw[1]

162 – ´Aliy bin al-Ja´d al-Jawhariy ametuhadithia: al-Mubaarak bin Fadhwaalah amenikhabarisha, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:

”´Utbah bin Ghazwaan (Radhiya Allaahu ´anh) aliwatolea watu Khutbah Baswrah na akasema: ”Nilikuwa mtu wa saba kusilimu pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), punde kidogo kabla ya mwezi wa Ramadhaan. Hatukuwa na chakula isipokuwa majani ya miti, mpaka vinywa vyetu vikaumia kwa sababu ya kula miti. Nilipata joho, nikaigawa mara mbili na nikampa kipande kingine Sa´d bin Maalik[2].”

163 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid, kutoka kwa Qays, kutoka kwa Sa´d bin Abiy Waqqaas, ambaye amesema:

”Tulikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kipindi ambacho ilikuwa chakula chetu pekee kilikuwa majani ya mizabibu na majani ya mshita. Kiasi cha kwamba tunapomwaga kinyesi chetu kinakuwa kama cha mbuzi; bila kuchanganywa kabisa.”

164 – Khaalid bin Khidaash ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa ´Aliy bin Zayd, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin Sufyaan al-Kilaabiy, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ee adh-Dhwahhaak, unakula nini?” Akasema: ”Nyama na maziwa.” Akasema: ”Kisha baadaye inakuweje?” Akasema: ”Kile ambacho tayari unakijua.” Akasema: ”Hakika Allaah (´Azza wa Jall) ameipigia mfano dunia kwa kile kinachomtoka mwanadamu.”

[1] Tamtam iliyotengenezwa kwa tende na siagi. 

[2] Bi maana Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 104-107
  • Imechapishwa: 25/07/2023