30. Ibn ´Uthaymiyn kuhusu al-Albaaniy

Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

“Yale ninayojua kuhusu Muhaddith wa Shaam na muheshimiwa Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy kupitia zile mara chache tulizokutana naye, ni kwamba ni mtu mwenye pupa kwelikweli wa kuitendea kazi Sunnah na kupambana na Bid´ah, ni mamoja katika ´Aqiydah na matendo. Ama kupitia usomaji wangu wa vitabu vyake nimeliona hilo pia, kwamba ana elimu ilio pana katika Hadiyth, inapokuja katika mapokezi na maana zake. Kupitia vitabu vyake Allaah (Ta´ala) amenufaisha elimu za waislamu, mifumo na kuielekea kwao elimu ya Hadiyth. Huu ni ushindi mkubwa kwa waislamu.

Swalah na salaam zimwendee bwana na Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wake wote.

Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy

1418-09-30

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 56
  • Imechapishwa: 05/12/2018