Hukumu ya ngamia, mbuzi, kondoo au ng´ombe aliyeokotwa

Swali: Alikuja ngamia ambapo akajiingiza na ngamia zangu. Nimejaribu kumfukuza mara nyingi lakini pasi na mafanikio. Hivi sasa ana miaka mine na nimemwacha na ngamia wangu ambapo anakula na kunywa pamoja nao. Nimemtangaza masokoni na vijijini lakini hata hivyo sikumtambua mmiliki. Ni ipi hukumu?

Jibu: Mkadirie thamani yake au muuze na utoe swadaqah kwa thamani yake au kwa kile kiwango ambacho utakuwa umekadiria kuwapa mafukara kwa nia thawabu zimwendee mmiliki. Hiki ndicho ambacho unaweza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/940
  • Imechapishwa: 05/12/2018