28. Tofauti kati ya washirikina wa kale na wa sasa II

2 – Washirikina wa kale walikuwa wakishirikisha wakati fulani na wakimwabudu Allaah pekee wakati mwingine. Wakiwa katika kipindi cha raha basi ndipo wanafanya shirki. Kunapokuja matatizo na wakakumbwa na mawimbi basi humkumbuka Allaah na wakamtakasia ´ibaadah. Amesema (Ta´ala):

فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ

“Wanapopanda merikebu humwomba Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini, lakini anapowaokoa katika nchikavu, tahamaki hao wanamshirikisha.”[1]

Dini ni ´ibaadah.

Amesema (Ta´ala):

وَإِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فِي الْبَحْرِ ضَلَّ مَن تَدْعُونَ إِلَّا إِيَّاهُ ۖ فَلَمَّا نَجَّاكُمْ إِلَى الْبَرِّ أَعْرَضْتُمْ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ كَفُورًا

“Inapokuguseni dhara baharini hupotea wale mnaowaomba isipokuwa Yeye pekee. Pindi anapokuokoeni katika nchi kavu, mnakengeuka; mtu amekuwa ni mwingi wa kukufuru.”[2]

[1] 29:65

[2] 17:67

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 152
  • Imechapishwa: 15/03/2023