28. Kitu chenye kukufurisha kinaweza kuwa moja katika vitu vitatu

Kinacholengwa ni kwamba mtu akifanya kitu chenye kukufurisha matendo yake yanaporomoka. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kubadilisha dini yake muueni.”[1]

Amesema (Ta´ala) ndani ya Qur-aan tukufu:

وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Hakika umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka yataporomoka matendo yako na hakika utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[2]

وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا

”Tutayaendea yale waliyoyatenda katika matendo, Tutayafanya kuwa ni vumbi lililotawanyika.”[3]

Matendo hayanufaishi kitu yakiambatana na shirki. Bali yanakuwa ni kama vumbi lililotawanyika. Amesema (Ta´ala):

وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Lau wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.”[4]

Kwa kifupi ni kwamba mtu akifanya kitu chenye kukufurisha – cha kimaneno, kimatendo au cha kimoyo kama mfano kuwa na mashaka –  anakufuru. Haijalishi kitu hata kama atasema kuwa yeye anashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah lakini akawa na mashaka kama Pepo ni kweli au sio kweli, Moto ni kweli au si kweli, akawa na mashaka kama Allaah yuko juu ya mbingu au hayuko juu ya mbingu, Allaah yuko juu ya ´Arshi au hayuko juu ya ´Arshi, akawa na mashaka juu ya utume wa Muhammad, akasema kuwa yeye hajui kama ni Mtume au si Mtume, akawa na mashaka juu ya utume wa Mtume yeyote ambaye ametajwa na Allaah ndani ya Qur-aan, akaona kuwa ni halali kumuoa dada, shangazi yake, mama yake mdogo, anakufuru kwa sababu amemkadhibisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sunnah ni kwamba yule mwenye kitenguzi miongoni mwa vichenguzi vya Uislamu anakufuru na matendo yake yote kama swalah, swawm na hajj yanabatilika. Amesema (Ta´ala):

وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Lau wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.”[5]

وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

”Yeyote atakayekanusha imani, basi yameporomoka matendo yake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[6]

Hapa ni pahali ambapo waislamu wameafikiana. Lakini waabudu makaburi hawaelewi. Waabudu makaburi na waabudia mawalii wako upofuni.

Haya ni mambo ambayo Shaykh (Rahimahu Allaah) aliyabainisha katika zama zake ambapo wakampinga na kusema kwamba eti Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab anawakufurisha waislamu na kwamba amekuja na dini mpya. Hivi ni kutokana na ujinga wao, upotofu wao na uchache wa elimu. Hakuleta dini mpya. Lakini ameleta yale yaliyosemwa na Allaah na Mtume Wake na yale waliyopita juu yake Maswahabah na waislamu. Allaah amjaze kheri.

[1] al-Bukhaariy (2016).

[2] 39:65

[3] 25:23

[4] 06:88

[5] 06:88

[6] 05:05

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 25/10/2021