27. Yanayofaa kwa mfungaji: Kikongwe na mwenye maradhi sugu wasioweza kufunga kulisha chakula badala ya kufunga

7 – Mzee mtumzima mwanaume na mwanamke na vivyo hivyo mgonjwa mwenye maradhi yasiyotarajiwa kupona watakula na kila mmoja wao atatakiwa kulisha masikini kwa kila siku iliyowapita. Hapa ni pale ambapo hawawezi kufunga kwa mujibu wa maoni ya  wanazuoni wengi. Wamesema japokuwa Aayah yenye kusema:

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ

”Kwa wale wanaoiweza lakini kwa tabu watoe fidia.”[1]

imefutwa, lakini hata hivyo hukumu ya kulisha bado ni yenye kuendelea kufanya kazi kwa mzee na kwa mgonjwa ambaye maradhi yake si yenye kutarajiwa kupona.

[1] 02:184

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 22/04/2023