28. Yanayofaa kwa mfungaji: Kumfungia maiti anayedaiwa

8 – Inapendeza kwa ndugu kuwafungia maiti wao. Inasihi kuwafungia. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kufa na anadaiwa swawm, basi amfungie walii wake.”[1]

Akitaka atamtolea chakula kwa kila siku moja aliyokuwa anadaiwa. Kwa hivyo ndugu huyu wa maiti amekhiyarishwa baina ya kumfungia na kumtolea chakula.

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

[1] al-Bukhaariy (1952) na Muslim (1147).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 45
  • Imechapishwa: 22/04/2023