27. Kusoma kwa sauti na kimya kimya katika swalah tano na nyenginezo

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma kwa sauti katika Fajr na katika zile Rak´ah mbili za mwanzo za Maghrib na ´Ishaa’. Dhuhr, ´Aswr, ile Rak´ah ya mwisho ya Maghrib na zile Rak´ah mbili za mwisho za ´Ishaa’ akisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kunyamaza[1].

Walikuwa wakiweza kutambua kusoma kwake kwa ukimya kwa kutikisika ndevu zake[2] na wakati mwingine akiwasikilizisha baadhi ya Aayah.

Alikuwa vilevile akisoma kwa sauti wakati wa swalah ya ijumaa, swalah za ´iyd, swalah ya mvua na swalah ya kupatwa kwa jua[3].

[1] Waislamu wameafikiana juu ya hili katika historia nzima. Vilevile kuna Hadiyth Swahiyh na za wazi zinazothibitisha hayo, kama alivyosema an-Nawawiy. Baadhi yake zitafuatia. Tazama ”al-Irwaa´”” (345).

[2] al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[3] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 93-94
  • Imechapishwa: 04/02/2017