Kuna aina mbili ya makatazo:

1 – Makatazo kwa njia ya uharamu. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ

“Na wala msiikaribie zinaa.”[1]

Kwa hivo unajiepusha na uzinzi hali ya kumuogopa na kumtukuza Allaah na pia kutaraji malipo Yake. Hivyo unakuwa ni mwenye kumwabudu Allaah kwa kule kujizuilia kwako kutokamana na uzinzi.

2 – Makatazo kwa njia ya mapendezo. Mfano wa hilo ni kama makatazo ya kuzungumza baada ya swalah ya ´Ishaa. Makatazo haya ni kwa njia ya mapendekezo. Kwa hiyo ukiacha mazungumzo baada ya swalah ya ´Ishaa kwa ajili ya kutekeleza amri yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) unakuwa ni mwenye kumwabudu Allaah kwa kufanya hivo.

Hizi ndio aina za ´ibaadah zilizoamrishwa na zilizokatazwa. Ni mamoja maamrisho hayo ni kwa njia ya ulazima au ya mapendekezo. Ni mamoja pia makatazo hayo ni kwa njia ya ulazima au ya mapendekezo. Unatakiwa kufanya maamrisho na kujiepusha na makatazo hali ya kumtii Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 17:32

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 44
  • Imechapishwa: 06/02/2023