Kuna aina mbili ya maamrisho:

1 – Miongoni mwa mambo aliyoamrisha Allaah kwa njia ya ulazima ni kama kusimamisha swalah. Amesema (Ta´ala):

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ

“Simamisheni swalah.”[1]

Kwa hivyo hiajuzu kumtekelezea swalah mwingine asiyekuwa Allaah. Mtu akimswalia asiyekuwa Allaah amefanya shirki.

Miongoni mwa mambo aliyoamrisha Allaah kwa njia ya mapendekezo ni kutumia Siwaak. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Lau nisingechelea kuwatia uzito ummah wangu basi ningewaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah.”[2]

Siwaak ni ´ibaadah inayopendeza. Mtu anatumia Siwaak hali ya kumwabudu Allaah. Kwa hivyo mtu asitumie Siwaak hali ya kuabudu kwa mwingine asiyekuwa Allaah.

[1] 02:43

[2] al-Bukhaariy (887) na Muslim (252).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 44
  • Imechapishwa: 06/02/2023