25. Muumbaji wa viumbe ndiye anastahiki kuabudiwa

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mola ndiye Mwabudiwa. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu Ambae amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na ucha Mungu. Ambaye amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa na akateremsha kutoka mbinguni maji, akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Hivyo basi msimfanyie Allaah washirika na hali ya kuwa nyinyi mnajua.”[1]

Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema:

“Muumbaji wa vitu hivi ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa.”[2]

Mfano wa aina za ´ibaadah ambazo Allaah ameamrisha:

MAELEZO

Mola ndiye mwabudiwa. Maana ya maneno Yake (Ta´ala):

رَبَّكُمُ

”… Mola wenu… ”

bi maana mwabudiwa wenu. Yeye ndiye anastahiki kuabudiwa. Kwa sababu Yeye ndiye kawalea viumbe kwa neema Zake. Yeye ndiye kawaumba. Yeye ndiye mwabudiwa.

Hii ndio Aayah ya kwanza ndani ya Qur-aan inayoamrisha Tawhiyd na sambamba na hilo ikakataza shirki:

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

”Hivyo basi msimfanyie Allaah washirika na hali ya kuwa nyinyi mnajua.”

Bi maana wanaolingana Naye na washirika ambao mnawatekelezea ´ibaadah.

Maneno ya mtunzi (Rahimahu Allaah):

”Mfano wa aina za ´ibaadah ambazo Allaah ameamrisha.”

Miongoni mwa fadhilah za Allaah kwa waja ni kwamba amewawekea aina ya ´ibaadah mbalimbali ambazo wanajikurubisha kwazo mbele Yake. Mtu hajui ni kwa aina ya ´ibaadah ipi ataingia kwayo Peponi.

[1] 02:21-22

[2] Tafsiyr Ibn Kathiyr (01/103).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 43
  • Imechapishwa: 06/02/2023