al-Hasan amesema:

“Kuna sampuli mbili za elimu. Elimu inayokuwa ulimini. Elimu hiyo ni hoja ya Allaah dhidi ya mtu. Elimu inayokuwa moyoni. Hiyo ndio elimu yenye manufaa.”

Salaf walikuwa wakisema:

”Kuna aina tatu ya wanazuoni: mwanachuoni anayemjua Allaah na maamrisho ya Allaah, mwanachuoni anayemjua Allaah lakini si mwenye kujua maamrisho ya Allaah na mwanachuoni anayejua maamrisho ya Allaah lakini hamjui Allaah.”

Mkamilifu wao zaidi ni yule wa kwanza. Naye ni yule anayemcha Allaah na anazitambua hukumu Zake. Shani ni kule mja kuitumia elimu yake kumtambua Mola wake. Anapomtambua Mola wake, basi hakika amempata karibu Naye. Pale atapompata karibu Naye, basi atamkurubia na kuitikia du´aa zake. Imekuja katika upokezi wa ki-israaiyl:

”Mwanadamu! Nitafute utanipata. Ukinipata, basi umepata kila kitu. Na ukinikosa, basi umekosa kila kitu. Na mimi ni Mwenye kupendwa zaidi kwako kuliko kila kitu.”

Dhuun-Nuun alikuwa akiyarudirudi maneno haya usiku:

Jitafutieni kile ambacho

mimi nimekipata

Hakika nimejipatia jengo

isiyokuwa na eneo la nje

Nikijiweka mbali, Ananikuurbia

au nikimkurubia, Anakuwa karibu

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema kuhusu Ma´ruuf:

”Anao msingi wa elimu; khofu juu ya Allaah.”

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 27/09/2021