26. Inafaa kwa mtu aliyejitwahirisha kwa Tayammum kupangusa juu ya soksi wakati anapotawadha?

Swali 26: Mtu akijitwahirisha kwa kufanya Tayammum na akavaa soksi za ngozi inafaa kwake kupangusa juu yake yakipatikana maji?

Jibu: Haijuzu kwake kupangusa juu ya soksi za ngozi ikiwa twahara yake ni ya aina ya Tayammum. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nilizivaa nikiwa katika hali ya twahara.”

Twahara ya Tayammum haina mafungamano yoyote na mguu. Ni twahara iliyo na mafungamano na uso na viganja vya mikono tu. Kujengea juu ya hili, ikiwa mtu hana maji au ni mgonjwa na hawezi kutumia maji wakati wa kutawadha, basi avae soksi za ngozi ijapo hana twahara. Atabaki nazo kwa muda usiokuwa maalum mpaka pale atapopata maji au mpaka pale atakapopona. Kwa mguu hauna mafungamano yoyote na twahara ya Tayammum.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/174)
  • Imechapishwa: 06/05/2021