25. Je, kuna tofauti kati ya kupangusa juu ya soksi za ngozi na kupangusa juu ya kitata?

Swali 25: Je, kuna tofauti kati ya kupangusa juu ya soksi za ngozi na kupangusa juu ya kitata?

Jibu: Ndio, kuna tofauti ikiwa ni pamoja na:

Tofauti ya kwanza: Kupangusa juu ya soksi za ngozi kumewekewa muda maalum ilihali kufuta juu ya kitata inafaa kwake kufanya hivo midhali bado ni mwenye kuihitajia.

Tofauti ya pili: Kitata hakifupiki na kiungo maalum ilihali soksi za ngozi zimefupika na miguu.

Tofauti ya tatu: Kupangusa juu ya soksi za ngozi kumeshurutishwa awe amezivaa akiwa na twahara tofauti na kitata.

Tofauti ya nne: Kupangusa juu ya kitata kunakuwa wakati wa hadathi ndogo na hadathi kubwa tofauti na soksi za ngozi. Pindi mtu ambaye amefungwa banzi analazimika kuoga basi anatakiwa kupangusa juu yake kama anavopangusa wakati anapotawadha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/174)
  • Imechapishwa: 06/05/2021