Swali 24: Je, ni lazima kupangusa kitata chote?

Jibu: Ndio, apanguse yote. Kimsingi ni kuwa mwili una hukumu ileile ya kile kitu cha mbadala muda wa kuwa Sunnah haijaonesha kinyume chake. Hapa upangusaji unachukua nafasi ya kuosha. Kama jinsi kuosha ni wajibu kueneza maji kiungo kizima vivyo hivyo ni lazima kupangusa kitata chote.

Ama kupangusa juu ya soksi za ngozi, ni ruhusa ambayo Sunnah imethibiti kuonyesha kuwa inatosheleza kupangusa sehemu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/173)
  • Imechapishwa: 06/05/2021