23. Je, ni lazima kukusanya kati ya Tayammum na kupangusa juu ya kitata?

Swali 23: Je, ni lazima kukusanya kati ya Tayammum na kupangusa juu ya kitata?

Jibu: Si lazima kukusanya kati ya mawili hayo. Kuwajibisha twahara mbili juu ya kiungo kimoja ni jambo linakwenda kinyume na misingi ya Shari´ah. Ni lazima kusafisha kiungo hichi kwa kutumia njia moja. Ama kuwajibisha kukisafisha kwa twahara mbili ni jambo lisilokuwa na mfano katika Shari´ah. Allaah hamfaradhishii mja ´ibaadah mbili ambayo sababu yake ni moja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/173)
  • Imechapishwa: 06/05/2021