22. Je, imeshurutishwa kupangusa juu ya kitata kisiwe kimefunika zaidi ya vile mtu anavohitajia?

Swali 22: Je, imeshurutishwa kupangusa juu ya kitata kisiwe kimefunika zaidi ya vile mtu anavohitajia?

Jibu: Haifai kupangusa juu ya kitata isipokuwa wakati wa haja. Ni lazima kuikadiria kwa makadirio yake. Haja haikufupika yale maeneo ya maumivu au ya donda peke yake. Kila ile sehemu inayohitajika ili kitata au plasta hii iwe imara basi ni haja. Ikiwa mtu amevunjika kwenye kidole lakini kukahitajika kufunga kidole kizima, basi hiyo ni haja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/173)
  • Imechapishwa: 06/05/2021