25. Yanayofaa kwa mfungaji: Kula kwa bahati mbaya baada ya kupambazuka alfajiri

5 – Mwenye kula au kunywa hali ya kuwa na mashaka juu ya kuchomoza kwa alfajiri na hakubainikiwa na kupambazuka kwake, basi funga yake ni sahihi na si lazima kulipa siku hiyo. Amesema (Ta´ala):

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi.”[1]

Ama kuhusu aliyekula au kunywa hali ya kuwa na mashaka juu ya kuzama kwa jua na haikubainika kwake kwamba limezama kweli na wala hakuwa na dhana yenye nguvu kwamba limezama, itampasa kuilipa siku hiyo. Kwa sababu kimsingi ni kwamba mchana bado unaendelea.

[1] 02:187

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 43
  • Imechapishwa: 22/04/2023