25. Tofauti ya washirikina wa kale na wa sasa katika kuelewa maana ya ´mungu`

Hawamaanishi ya kwamba mungu ni yule mwenye kuumba, mwenye kuruzuku na mwenye kuyaendesha mambo. Kwa kuwa wao wanajua ya kwamba hayo ni ya Allaah pekee, kama tulivyotangulia kusema. Mungu wanayemaanisha ni yule ambaye washirikina wa zama zetu wanamaanisha kwa kusema “bwana”.

MAELEZO

Mungu kwa mujibu wa washirikina wa mwanzo hakuwa yule anayeumba, mwenye kuruzuku na mwenye kuyaendesha mambo. Kwa kuwa hii ni maana ya mola. Kuna tofauti kati ya maana ya mola na mungu. Kuna tofauti kati ya Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. ´Mungu` waliekuwa wanamkusudia washirikina ni yule ambaye washirikina wa kipindi cha mtunzi wa kitabu waliyekuwa wanamkusudia kwa neno ´bwana`. Haya yanapatikana mpaka hii leo wale wanaowaomba na kujikurubisha kwao wanawaita kuwa ni mabwana zao kama mfano wa bwana al-Badawiy, bwana ar-Rifaa´iy, bwana at-Tiyjaaniy na wengineo. Wanaamini kuwa mabwana hawa wana nafasi mbele ya Allaah inayowawezesha kuweza kuombea mbele ya Allaah na inayowawezesha vilevile kuwaomba badala ya Allaah au kuwachinjia, kuwawekea nadhiri, kutufu kwenye makaburi yao na kutabaruku kwayo. Washirikina wa kale walikuwa wakiyaita mambo haya kuwa ni ´mungu` na washirikina waliokuja nyuma wanayaita mambo haya kuwa ni ukati kati, njia, uombezi na majina mengine yenye kubadilisha uhakika wa mambo. Ni waungu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 40
  • Imechapishwa: 09/11/2016