25. Maadui wa Tawhiyd na elimu, vitabu na hoja zao

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Na yawezekana maadui wa Tawhiyd wakawa na elimu kubwa, vitabu na hoja. Kama alivyosema Allaah (Ta´ala):

فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرِحُوا بِمَا عِندَهُم مِّنَ الْعِلْمِ

“Basi walipowajia Mtume wao kwa hoja za wazi, walifurahia kwa yale waliyokuwa nayo katika elimu.” (40:83)

MAELEZO

Inawezekana maadui wa Mitume ambao wanajadiliana nao na kuwakadhibisha, wana elimu kubwa, vitabu na hoja tata wanazoziita kuwa ni “hoja”. Wanawapaka watu mchanga wa machoni ambapo wanawachanganyia watu haki na batili. Amesema (Ta´ala):

فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرِحُوا بِمَا عِندَهُم مِّنَ الْعِلْمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ

“Basi walipowajia Mtume wao kwa hoja za wazi, walifurahia kwa yale waliyokuwa nayo katika elimu na yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.” (40:83)

Furaha kama hii ni yenye kusemwa vibaya, kwa sababu Allaah haridhishwi nayo.

Kwa sentesi hii anaashiria mtunzi (Rahimahu Allaah) ya kwamba inatupasa kutambua elimu na utata wa watu hawa. Lengo ni ili tuweze kuwaraddi kwa silaha zao wenyewe. Haya ni katika uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alipomtuma Mu´aadh Yemen alimwambia:

“Hakika wewe unawaendea watu katika Ahl-ul-Kitaab.”[1]

Alisema haya ili aweze kujiandaa kwa ajili yao na ajue ni kitabu kipi walichonacho, ili baada ya hapo aweze kuwaraddi kwa kile wanachojadili kwacho.

[1] al-Bukhaariy (4347) na Muslim (29).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 48
  • Imechapishwa: 14/10/2023