Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa tano

Maadui wa Mitume na Manabii

Na jua kwamba Allaah (Subhaanah) kwa hekima Yake hakutuma Mtume kwa Tawhiyd hii isipokuwa alimuwekea maadui. Kama alivyosema Allaah (Ta´ala):

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا

“Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabii maadui mashaytwaan katika watu na majini wakidokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya udanganyifu.” (06:112)

MAELEZO

Katika sentesi hii mtunzi (Rahimahu Allaah) amezindua faida moja kubwa sana. Ni pale anaposema kuwa Allaah (´Azza wa Jall) hakumtuma Mtume yeyote, isipokuwa alimfanya kupata maadui katika watu na majini. Uwepo wa adui unasambaratisha na haki inabainika. Kila mbavyo kuna mpinzani, ndivyo jinsi hoja ya upande mwingine inakuwa na nguvu zaidi. Haya ambayo Allaah (Ta´ala) amewajaalia Mitume, amewajaalia hali kadhalika wafuasi wao. Wafuasi wao wanafikwa na yale yenye kuwafika Mitume. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا

“Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabii maadui mashaytwaan katika watu na majini wakidokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya udanganyifu.” (06:112)

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا مِّنَ الْمُجْرِمِينَ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيًا وَنَصِيرًا

“Na hivyo ndivyo Tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wahalifu. Na Mola wako anatosheleza kuwa ni Mwenye kuongoa na Mwenye kunusuru.” (25:31)

Wahalifu hawa wanawafanyia uadui Mitume, wafuasi wao na yale wanayoyafikisha kwa njia mbili:

1 – Kueneza shaka.

2 – Uadui.

Kuhusiana na shaka, Allaah (Ta´ala) amesema:

وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيًا

“… na Mola wako anatosheleza kuwa ni Mwenye kuongoa… “

Bi maana yule ambaye maadui wa Mitume wanataka kumpotosha.

Ama kuhusu uadui, Allaah (Ta´ala) amesema:

وَنَصِيرًا

“… na Mwenye kunusuru.” (25:31)

Bi maana yule ambaye maadui wa Mitume wanataka kumzuia.

Allaah (Ta´ala) anawaongoza Mitume na wafuasi wao na anawanusuru juu ya maadui zao, pasi na kujali ni nguvu kiasi gani adui atakuwa nazo. Ndio maana tusikate tamaa kutokana na wingi wa maadui na ile nguvu walionayo kupambana na haki. Haki ni kama alivyosema Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah):

Haki ni yenye kunusuriwa na kadhalika ni yenye kutahiniwa

usishangae – hii ni njia ya Mwingi wa rehema

Haijuzu kwetu kuvunjika moyo. Badala yake ni juu yetu kukusanyika juu ya kuwa na moyo na kusubiri. Mwisho mwema ni kwa wale wamchao Allaah. Kujipa moyo ni miongoni mwa sababu kubwa za kuwalingania watu katika Uislamu na kupigania mafanikio yake, kama ambavyo kukata tamaa ni miongoni mwa sababu za ulinganizi kufeli na kurudi nyuma.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 14/10/2023