23. Witr ya Tarawiyh mwishoni mwa Ramadhaan

Swali: Kuhusu Witr ya Tarawiyh mwishoni mwa Ramadhaan. Je, niswali Witr na nilale au niicheleweshe pamoja na kisimamo cha mwishoni mwa usiku kwa sababu mimi hulala kati ya muda wa Tarawiyh na kisimamo cha usiku?

Jibu: Ukiswali na imamu swalah ya Tarawiyh basi bora ni wewe kuswali Witr pamoja naye ili upate ujira kamilifu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayesimama pamoja na imamu mpaka akamaliza basi anaandikiwa kuwa ameswali usiku mzima.”[1]

Ukiamka mwishoni mwa usiku na ukataka kuswali basi swali kile kitachokuwa wepesi kwako pasi na Witr. Kwa sababu hakuna Witr mbili katika usiku mmoja kama ilivyokwishatangulia. Ukiacha Witr mwanzoni mwa usiku au Witr ukaifanya shufwa kwa kuongeza Rak´ah moja mwanzoni au mwishoni mwa usiku ili uweze kuswali Witr mwishoni mwa usiku ni sawa pia.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

[1] Abu Daawuud na at-Tirmidhiy.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 15/04/2022