Swali: Ni ipi hukumu ya kusafisha meno kwa Siwaak katika Ramadhaan?

Jibu: Inafaa kutumia Siwaak katika Ramadhaan nzima, ni mamoja michana na nyusiku zake. Ibn Rabiy´ah amesema:

“Mara zisizohesabika na kudhibitika nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitumia Siwaak ilihali amefunga.”[1]

[1] Abu Daawuud (2364) na at-Tirmidhiy (725).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 25
  • Imechapishwa: 24/03/2022