23. Imaam ´Abdil-Wahhaab na wanafunzi wake walikuwa katika njia ya Salaf

Ambaye atazingatia zile dalili alizoziandika Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) na wanafunzi wake basi ataona haki, hoja na dalili zenye kung´aa zinazoweka wazi upotofu wa maneno ya wapinzani na hoja zao tata. Vilevile itabainika haki kwa dalili zake za wazi.

Wao (Rahimahumu Allaah) – licha ya kuchelewa zama zao – wamewafikishwa kuidhihirisha haki na kubainisha dalili zake na pia wakabainisha yale yanayohusiana na ulinganizi wa Tawhiyd, kuwaraddi walinganizi wa mizimu na waabudia makaburi na wakasimama msitari wa mbele katika njia hii. Walikuwa juu ya njia ilionyooka – njia ya Salaf-us-Swaalih. Walitaka msaada katika mlango huu kwa dalili za wazi zilizotajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah, vitabu vya Hadiyth, vitabu vya tafsiri ya Qur-aan. Walipita katika mwenendo huo mpaka Allaah akaidhihirisha haki na kuitweza batili kupitia wao na akawafanya wao wakawasimamishia hoja wengine, wakaeneza bendera ya Uislamu, ikanyanyuka bendera ya Jihaad na Allaah akajaalia baraka na fadhilah zisizohesabika kupitia wao. Watu wa haki katika miji yote waliojua vitabu vyao, usahihi wa ulinganizi wao na kusalimika kwa mfumo wao wakawa wanaeneza ulinganizi wao na wanataka msaada kwa yale waliyoandika katika jambo hili dhidi ya wapinzani na maadui wa Uislamu walioko mahali kote miongoni mwa watu wa shirki, Bid´ah na makhurafi.

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 18/05/2022