48. Funga pamoja na wengine ijapo ni siku 31

Swali 48: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye mwanzoni mwa mwezi alifunga na Saudi Arabia kisha akasafiri katika nchi ambayo mwezi mwandamo wake ulichelewa  nasi – je, afunge siku thelathini na moja[1]?

Jibu: Afunge pamoja nao na afungue pamoja nao ijapo masiku yake yatazidi. Hayo ni kutokana na Hadiyth iliyokwishatangulia:

“Fungeni siku wengine wanafunga, fungueni siku wengine wanafunga na chinjeni siku wengine wanachinja.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/155).

[2] at-Tirmidhiy (697).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 18/05/2022