49. Mwenye kula daku katika nchi na kukata swawm katika nchi nyingine

Swali 49: Ni ipi hukumu ya mwenye kula daku katika nchi moja na akafungua katika nchi nyingine mfano wa yale yaliyonitokea ambapo nilikula daku katika nchi fulani katika Ramadhaan mwaka uliopita na siku hiyohiyo nikafika Riyaadh na nikafutari pamoja na watu wa Riyaadh pamoja na kuzingatia kwamba ipo tofauti ya saa moja katika muda kati ya Riyaadh na nchi yangu. Je, nalazimika kulipa siku hiyo[1]?

Jibu: Hapana vibaya kufanya hivo. Kwa sababu yuko na hukumu ya ile nchi ambayo anakula daku na kufutari ndani yake. Haimdhuru kitu kule kutofautiana kati ya nchi mbili hizo inapokuja katika urefu wa mchana na ufupi wake na kutangulia mbele kwa Maghrib na kuchomoza kwa Fajr na kuchelewa kwake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/321-322).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 66
  • Imechapishwa: 18/05/2022