Ambaye atazingatia hali za wanazuoni waliowafikishwa ambao ni wabobeaji katika Ummah huu na akazingatia Qur-aan na Sunnah na wakajifunza yale yatakayowasaidia kuvifahamu viwili hivo ufahamu sahihi wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na wale waliowafuata kwa wema katika maimamu wa Uislamu katika yale waliyoandika na yaliyonukuliwa kutoka kwao na wale waliopita juu ya njia yao katika watu wa kweli, waaminifu na wenye utambuzi; kama mfano wa Abul-´Abbaas bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) na mwanafunzi wake ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim, Haafidh Ibn Kathiyr na wengineo waliojitokeza katika uwanja huu katika maimamu wa shani hii, yule ambaye atazingatia hali zao na Allaah akamfungulia kuyafahamu yale waliyoyasema na waliyoyaandika basi ataona maajabu na mafunzo makubwa, elimu sahihi, nyoyo zenye kung´aa na hoja zinazong´aa ambazo zinamwelekeza yule mwenye kushikamana nazo katika njia yenye furaha na njia ilionyooka. Kwa hayo, baada ya kuwafikishwa na Allaah, kuhakikisha lengo linalotakiwa na kuikinga nafsi yake kwa elimu, utambuzi na utulivu katika haki ambayo Allaah amewatumiliza kwayo Mitume Yake, akateremshwa kwayo Vitabu Vyake na wakapita juu yake Salaf wa Ummah huu. Vielevile itambainikia kwamba wale walinganizi waliopinda na walinganizi wapotofu waliokwenda kinyume nao hawana jengine isipokuwa hoja tata za batili ambazo hazifidishi chochote.

Mwanafunzi wa kikweli ni yule awezaye kupambanua haki kutokamana na batili kwa dalili zilizo wazi na hoja zake zenye kung´aa, anasoma vitabu vya maimamu waongofu, anachukua kutoka humo yale yaliyoafikiana na haki, anayaacha yale ambayo kumedhihiri ubatilifu wake na hayakuafikiana na haki.

Miongoni mwa maimamu hawa walioshuhurika ni Shaykh na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) na wasaidizi wake katika karne ya kumi na mbili na kuendelea mbele. Wamefaulu katika uwanja huu, wakaandika vitabu vitukufu na vyenye mafanikio, akawatumia vitabu watu mbalimbali na akawajibu wapinzani wake na akaiweka haki wazi ndani ya vitabu na tungo zake kwa dalili kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah. ´Allaamah na Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Qaasim (Rahimahu Allaah) amekusanya kiasi kikubwa katika hayo katika kitabu chake kinachoitwa “ad-Durar as-Saniyyah fiyl-Ajwibah an-Najdiyyah”.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 18/05/2022