22. Washirikina wa kale walikufuru kwa yote mawili

Wakisema kuwa hawawaabudu kwa sababu hawasemi kuwa ni mabanati wa Allaah na kwamba eti washirikina wa kale walishirikisha kwa sababu walikuwa wanaona kuwa Malaika ni wasichana wa Allaah na kwamba wao hawaonelei hivo na kwamba shirki yao haikuwa katika kuwaomba na kwamba walishirikisha pale waliposema kuwa ni wasichana wa Allaah na kwamba ni wana wa Allaah, wakatalie hilo na waambie kwamba walikufuru kwa yote mawili. Kila kimoja katika hayo ni shirki yenye kujitegemea. Mwenye kumnasibishia Allaah mtoto ni shirki yenye kujitegemea. Vilevile kuwaomba na kuwataka msaada ni kufuru yenye kujitegemea. Washirikina walikusanya yote mawili. Hivyo ukiwaomba pamoja na Allaah na ukawataka msaada basi umetumbukia kwenye shirki. Haijalishi kitu hata kama hukusema kwamba Malaika ni wasichana wa Allaah, kwamba al-´Uzayr ni mwana wa Allaah na kwamba al-Masiyh ni mwana wa Allaah. Kuwafanyia ´ibaadah kwa kuwaomba uokozi na kuwawekea nadhiri ni shirki. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.”[1]

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ

Ni nani aliyepotea zaidi kuliko yule anayemwomba badala ya Allaah, ambao hatowaitikia mpaka siku ya Qiyaamah nao hawatambui maombi yao. Na [Qiyaamah] watakapokusanywa watu [miungu ya uongo] watakuwa maadui wao na watakuwa kwa ‘ibaadah zao ni wenye kuzikanusha.”[2]

Ameita maombi yao kuwa ni ´ibaadah. Amesema (Ta´ala):

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۚ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ

“Huyo ndiye Allaah, Mola wenu, ufalme ni Wake pekee.  Wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatakuitikieni na siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu na wala hakuna atakayekujulisha vyyema kama Mwenye khabari zote.”[3]

Ameita maombi yao kuwa ni shirki. Amesema (Ta´ala):

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote mwenye kuomba du’aa pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake. Hakika hawafaulu makafiri.”[4]

Amewaita kuwa ni makafiri kwa kitendo chao cha kuwaomba Malaika, Mitume na waja wema japokuwa hawatosema kuwa ni wasichana wa Allaah. Kwa hivyo kumthibitishia Allaah mtoto ni kufuru yenye kujitegemea na kuwaomba Malaika, wafu na mawalii ni kufuru yenye kujitegemea. Kutukana dini ni kufuru yenye kujitegemea. Kuhalalisha yale aliyoharamisha Allaah, kama vile uzinzi, ni kufuru yenye kujitegemea. Kudondosha yale aliyoyawajibisha Allaah ni kufuru yenye kujitegemea. Kama mtu akasema kwamba swalah, hajj au zakaah sio wajibu ni kufuru yenye kujitegemea. Akikwambia:

[1] 72:18

[2] 46:05-06

[3] 35:13-14

[4] 23:117

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 20/10/2021