23. Makatazo ya kuwaomba mawalii pamoja na Allaah

Akikwambia kwamba:

إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

“Hakika mawalii wa Allaah hawana khofu juu yao na wala hawatohuzunika.”[1]

na kwamba Malaika na waja wema kama vile al-Laat ni miongoni mwa mawalii wa Allaah, itika umwambie:

 أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

“Mawalii wa Allaah hawana khofu juu yao na wala hawatohuzunika.”

kutokana na matendo yao mema. Lakini hiyo haina maana kwamba inafaa kuwaomba pamoja na Allaah. Ni kweli kwamba hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika na wana matendo yao mema. Lakini haifai kwako ukawaomba pamoja na Allaah. Haifai kwako ukawaomba msaada. Haifai kwako ukawaomba wakutatulie mahitajio yako na kukuondolea matatizo. Matendo yao ni ya kwao. Karama zao ni za kwao. Wana karama na matendo mema. Lakini hiyo haina maana kwamba inafaa ukawoamba na ukawashirikisha. Bali ni lazima kwako kuwapenda kwa ajili ya Allaah na kuwaiga katika mambo ya kheri. Lakini haifai kwako ukawaomba badala ya Allaah kama ambavyo haifai kwako ukawaomba Mitume na waja wema. Kusema kwamba ni mawalii wa Allaah ni haki. Lakini hili halipelekei wakaombwa pamoja na Allaah. Kama ambavyo Mitume na Manabii ni haki lakini haina maana kwamba inafaa wakaombwa pamoja na Allaah. Hawatakwi msaada.

Kwa haya inapata kubainika ubatilifu wa shubuha hii, kwamba washirikina wako katika upotofu wa mbali na wamepofoka kutoiona haki. Amesema (Ta´ala):

صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ

“Viziwi, mabubu, vipofu.”[2]

أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا

“Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au wanatia akilini? Si vyenginevyo isipokuwa ni kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia.”[3]

خَتَمَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰ أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ

”Allaah amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao na juu ya macho yao pana kizibo.”[4]

Wamepotea kuacha uongofu. Hawakuifahamu haki pamoja na kwamba Allaah (Ta´ala) ameibainisha:

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ

”Haiwi kwa Allaah awapotoze watu baada ya kuwa amewaongoa mpaka awabainishie ya kujikinga nayo.”[5]

Amewatumiliza Mitume ili waje kutoa bishara na kuonya na ameteremsha Vitabu ili vije kubashiria na kuonya. Lakini wanapuuza, wako mbali na kuyafahamu maandiko, kuyapokea, kuipokea haki na faida zake. Bali kilichoenea zaidi kwao ni kufuata matamanio yao na kuwafuata kichwa mchunga watangu wao.

[1] 10:62

[2] 02:18

[3] 25:44

[4] 02:08

[5] 09:115

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 20/10/2021