Makatazo ya kujifananisha na Ahl-ul-Kitaab katika kuleta mipasuko

Swali: Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ

“Wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakatofautiana baada ya kuwajia hoja ubainifu.”[1]

Aayah hii imewateremkia mayahudi na manaswara. Kadhalika tunaona kuwa Quraysh wakati alipowajia Mtume walitofautiana na wakafarikiana pamoja na kwamba hawana elimu kama walionayo mayahudi na manaswara. Walifuata mkondo uleule; walikataa kama walivyokataa Ahl-ul-Kitaab hawa.

Jibu: Mayahudi na manaswara ndio msingi wa shari. Walitofautiana baada ya kufikiwa na elimu. Ndipo Allaah akaukataza Ummah huu wasifanye kama matendo yao. Ama Quraysh na mfano wao hawakuwa na elimu. Allaah akawakataza Ummah wa Muhammad kutofautiana kama walivyotofautiana Ahl-ul-Kitaab baada ya wao pia kufikiwa na elimu. Walijiliwa na Tawraat na Injiyl lakini hata hivyo wakatofautiana na hawakutosheka na yale waliyoteremshiwa. Ama kuhusu tofauti za makafiri wa Quraysh hazina msingi wowote. Ni tofauti batili za wajinga. Hawakuwa na mategemezi yoyote.

[1] 03:105

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 18
  • Imechapishwa: 20/10/2021