22. Ni wajibu kusema Tasmiyah kabla ya kutawadha

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

Ni wajibu kusema “Bismillaah” mtu akikumbuka hilo.

MAELEZO

Ni lazima kusema “Bismillaah” wakati mtu atakumbuka. Shaafi´iyyah wanaona kuwa kusema hivo ni jambo limependekezwa na sio lazima. Endapo mtu ataacha kusema hivo kwa makusudi wudhuu´ wake unasihi. Hayo pia ndio maoni ya Maalik, Abu Haniyfah na kikosi kikubwa cha wanachuoni. Na ndio udhahiri wa mapokezi mawili ya Ahmad. Kuna upokezi mwingine umepokelewa kutoka kwake kwamba ni lazima[1].

[1] al-Majmuu´ (01/408).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 33
  • Imechapishwa: 15/12/2021